Mchungaji avamiwa na mamba wakati akifanya kazi ya kuwabatiza wafuasi wake


Kulingana na ripoti za BBC, Docho Eshete aliumwa miguuni na mikononi na mgongoni kabla ya kuaga dunia kutokana na majeraha hayo.


Mamba mmoja alimrukia mchungaji huyo aliyekuwa akiwabatiza wafuasi wake

-Mnyama huyo alijaribu kuubeba mwili wake lakini akazuiliwa na wavuvi waliokuwa na nyavu

Mchungaji mmoja kutoka Ethiopian aliuawa na mamba alipokuwa akiwabatiza wafuasi wake katika Ziwa Abaya.

Inasemekana mchungaji huyo alikuwa akiwabatiza watu 80 kabla ya kukutana na mauti yake Jumapili Juni 3.

Inasemekana wavuvi walimzuia mnyama huyo kutobeba mwili wa mchungaji huyo kwa kutumia nyavu zao.

No comments