NENO KUU MAKAMBINI LEO 30
SOMO: SISI SOTE TU WANA NA BINTI ZA MUNGU.
Trh 29 June 2021 jioni
Makambi-Tanga Jiji
Pr. Godwin Lekundayo
👌1 Yohana 3:1-2
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.
👌Kwa hakika mm na ww ni wana wa Mungu kwa ajili ufalme wake sasa na si kwa wakati ujao.
👌Mungu anaposema zishikeni amri ..maana yake ni utaratibu wa nchi ile . Na huwez kwenda uko bila kushika utaratibu wa nchi ile.
👌Yaani uende mbinguni bila mazoezi. Ata kumuona malkia tu wa dunia hii unafanya mazoezi pia ..je iweje mbingu? Fanya mazoezi ambayo ni amri za Mungu.
👌Yesu anazaliwa kwenye hori la ng'ombe penye hali mbaya ili kuonyesha kuwa Yesu ni kwa ajili ya watu wote yaani walio daraja la chini na la juu kimaisha.
👌Ujue watu walimuona Yesu kama wa kawaida sana.... Ila baadae aliwaponya viziwi, viwete n.k....hatimae wakamfanyia heshima ya kumdhalilisha msalabani. Yaani hata ww kuna watu wanajifanya hawakutambuiii na kukudhalilisha pia.
👌Wakati mwingine omba kimoyo moyo tu na Mungu wako sio upige makelele sijui Mungu uliyekausha bahari ya shamu ....kabla hujasema amina shetani nae huyooo. Hii himaanisha kuwa shetani anatutembelea kila mara hivyo si kila kitu asikiee, usieleze kila kitu kwa marafiki zako utaangamizwa mara tu wakisikia.
👌Hata baada y uasi kuingia edeni swali likawa ..je tumtume nani akamkomboe mwanadamu..? Yesu akajibu mm hapa nitume niende nkamfie mwanadamu....! Ujue hata malaika walishangaaa kusikia hii kauli kutoka kwa Yesu.
👌Hapakuwa na namna nyingine ya mwanadamu kuokolewa isipokuwa kujitoa kwake Yesu kufa kwa ajili yetu.
Luka 12:7
Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi.
✓Mungu anathamini sana kuliko viumbe vingine hivyo tusiogope.
Yeremia 1:5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
✓Mungu alikujua mapema kuwa utazaliwaje, utakulaje, utaishije, utalalje, utaoaje na kuolewaje n.k...ila onyo tusivuruge ratiba yake juu yetu afanye apendavyo maana yeye alitujua tangu mwanzo na mwisho wetu pia anaujua
Barikiweni
Post a Comment