Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 19

KESHA LA ASUBUHI

JUMAMOSI, JUNI, 19, 2021
SOMO: KILA MSHIRIKI NI MMISHENARI 

Naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia. 

Isaya 49: 6. 



Jumanne asubuhi, Juni 19. Nimeangalia kwenye saa yangu; ni saa nane kamili. Ninavaa nguo, ninamtafuta Bwana, na kujaribu kuandika maneno machache kwa ajili ya kutuma kwenda Afrika asubuhi hii. Naomba Bwana anisaidie katika kuandika kila mstari. 



Tazama Isaya 49. Siwezi kuandika sura hiyo nzima. Isome kwa makini na kwa dhati. Ni maneno mazuri kiasi gani! “Akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa” (Isaya 49:3). Ni wangapi baada ya kufanya kadiri wawezavyo, katika mazingira magumu sana, wakiteseka kwa mahitaji ya nyenzo na kuhitaji sana vitu, wapo tayari kusema, kwa maneno ya Maandiko, "Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina BWANA, na thawabu yangu ina Mungu wangu." (Fungu la 4). 



Maonyo yote yanapaswa kutolewa. Ukweli, ukweli wa Biblia, unapaswa utangazwe katika mikutano yetu mikubwa, na kanisa liweze kusikia ukweli. Wanayo fursa. Wote wanaweza wasitamani kusikia. Wengi wanapinga kila kitu ambacho kinawataka wajikane nafsi. Hawapo tayari kuikubali Sabato. Katika Kutoka 31:12—18 imeoneshwa wazi wazi kwa mistari iliyo wazi kile ambacho Mungu anatarajia kutoka kwa watu wake, na kukataa kwa kudhamiria matokeo yake ni kifo. Pamoja na hili, wengi watakataa kutii kwa sababu ukweli huu unahusisha kujikana nafsi na kujitoa kafara. 



Watumishi wa Mungu wengi hawatasikia na kushawishiwa. Hawataingia katika madhabahu ya ukweli ili kupokea maarifa ya ukweli wa Neno, lakini watauondoa ufunguo wa maarifa kutoka kwa watu kwa kupotosha Maandiko wakipambana na Neno la Mungu kulitoa katika maana yake halisi. Kwa hiyo kila hatua inayopigwa katika kuwafikia watu ili kuwaokoa wasipotee katika makosa na kutotii inahitaji pambano gumu lisilokoma. Je, litakoma? Hapana. Inua viwango. Pandikiza kumbukumbu za ukweli wa Mungu katika kila sehemu inayowezekana, fanya kazi katika maeneo mapya, na watu wataongoka. 



Baadhi ya watu ambao hawafanyi maamuzi mara moja watasaidia kuipeleka mbele kazi kwa uwezo wao na huruma zao, na wao wenyewe watakaa upande wa Bwana. Mungu atakuwa na wawakilishi katika kila sehemu pande zote za dunia. 



—Barua ya 86, Juni 19, 1900,, kwa A. 

Post a Comment

0 Comments