Advertisement

Responsive Advertisement

CCM YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KAUNDA

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Rais wa kwanza wa Zambia na aliyekuwa Kiongozi wa Chama cha United National Independent Party (UNIP) Mzee Kenneth David Kaunda kilichotokea  tarehe 17 Juni, 2021 katika Hospitali ya kijeshi ya Maina Soko iliyopo Lusaka nchini Zambia.

Mzee Kaunda aliyezaliwa tarehe 28 Aprili 1924 na kuliongoza Taifa la Zambia kuanzia mwaka 1964 ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza mpaka mwaka 1991, atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa viongozi wa Nchi tano zilizokuwa mstari wa mbele katika harakati za kupigania uhuru na ukombozi wa Bara la Afrika kutoka
kwa wakoloni akishirikiana kwa karibu na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

"Bara la Afrika limempoteza Kiongozi jasiri na shupavu aliyeanzisha na kuongoza harakati za kudai uhuru na ukombozi wa nchi ya Zambia pamoja na kusaidia nchi za Afrika kupata uhuru, akiunga mkono mapambano dhidi ya siasa za ubaguzi wa rangi popote duniani"Ndugu Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chama Cha Mapinduzi kimetuma salamu za pole kwa Rais wa Zambia Mhe Edga C Lungu,wananchi wa Taifa la Zambia wanachama wa Chama cha UNIP, familia ya Marehemu Mzee Kaunda pamoja na ndugu, jamaa na marafiki. 

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee Kannda mahali pema peponi. Amina.

(Via;@ccmtanzania)

Post a Comment

0 Comments