Advertisement

Responsive Advertisement

AMKA NA BWANA LEO 16

KESHA LA ASUBUHI

JUMATANO, JUNI, 16, 2021
SOMO: AJABU YA MSALABA 

Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 

1 Petro 1:18, 19. 



Hii ilikuwa siku njema kwa watu wa Iowa. Mkutano wetu ulifunzwa karibu saa saba kamili. Karama ya thamani ya wokovu na ukombozi kwa wale wote watakaokubali ilionekana kuwa ya kushangaza sana, ni ya juu sana kuliko ufahamu wetu, kiasi kwamba lugha haikuweza kuelezea baraka zisizokoma zilizoletwa kwetu na Mkombozi wa ulimwengu. Ukuu wake ulishuka kuja katika udhaifu wetu. 



Yesu, Mwokozi wa thamani! Tunaweza kuuelewa upendo wa Baba kupitia kumtoa Mwana Wake mpendwa ili afe kwa ajili ya ulimwengu uliopotea. Tunapojifunza upendo huu usioelezeka kwa kuangalia msalaba wa Kalvari, tunastaajabu sana, tunashangaa sana. Tunaona rehema, upole, na msamaha vikichanganywa kwa ukamilifu pamoja na haki na heshima na nguvu. Yesu anamsihi mwenye dhambi amtazame Yeye ili aishi. Anasema, “Nimepata fidia.” Ufa uliosababishwa na dhambi umeunganishwa kwa msalaba wa Kalvari. Roho zinazoamini zinaweza kumwomba Baba anayesamehe akitupatanisha Kwake kupitia msalaba wa Kalvari. 



Ujuzi juu ya Kristo hufunua vina vya dhambi na tabia yake ya hatia, wakati kwa njia ya imani tunaona kijito cha kusafisha, damu ya Kristo ambayo inasafisha kila doa, kila doa la dhambi. Wokovu huu hauthaminiwi nusu nusu. Wokovu tuliopewa kupitia damu ya Yesu hauthaminiwi kuwa wa thamani isiyo na kikomo. Kwa imani karama hii yapasa ikubaliwe kikamilifu kama zawadi kuu ya Mungu kupitia kwa Yesu Kristo. Mzigo wa dhambi zetu na huzuni zetu uliwekwa kwa Yule ambaye ni mwenye huruma kuweza kusamehe, na mwenye nguvu kuweza kuokoa. 



Kwa nini tunakuwa wa baridi sana? Kwa nini tunakuwa wa duniani? Kwa nini hatujali sana? Kwa nini upendo wa Yesu usiwake kwenye madhabahu ya mioyo yetu? Aliubeba mzigo wa dhambi zetu; kwa nini hatuna imani kubwa? Kwa nini hatumwamini kikamilifu na kupokea kwa imani kila kitu kutoka katika mkono ule uliopigiliwa misumari pale msalabani ili uweze kuwa na nguvu ya kuokoa? Kwa nini tusiuamini upendo huo ambao umeoneshwa kwetu katika kafara hiyo isiyo na kikomo ili tuweze kuishi? 



Utazame msalaba kwa imani. Utazame na uishi. Hili litakuwa ni somo na wimbo wetu milele zote



—Barua ya 6, Juni 16, 1881,, kwa Edson na Emma White.

Post a Comment

0 Comments