Advertisement

Responsive Advertisement

DEFENDING IS AN ART NA GEORGE AMBANGILE

Ufaransa ukiacha mafundi wengi , lakini wana nidhamu sana ya uzuiaji , kila mchezaji anajua kazi yake, wanacheza kwa pamoja , wanasaidiana, hawafanyi tackling zisizo za lazima , wanazuia nafasi vizuri ( nyuma ya kila mstari, na space za pembeni ) , wanafunga njia za pasi kwa haraka sana hasa pale wakipoteza mpira .

✍Ujerumani kuanza na ' Back 3 ' pamoja na viungo wawili technical katika ya uwanja iliwapa faida kukabiliana na pressing ( walijiandaa kwa hilo ) kutoka kwa Ufaransa. Wakianza nyuma shape ya 3-4 ( mabeki watatu nyuma , viungo wawili katika mstari mmoja na mawingback 2 jumla mstari una watu wanne ) ngumu kuwafanyia pressing ndio maana Ufarans walikuwa wanashuka chini .... walitaka kutengeneza mtego..upi ?

✍Ujerumani wakisogea mbele , space zilikuwa zinafunga nyuma ya mawingback wawili Gossens na Kimmich na pembeni ya Gundogan na Kroos na hapo ndio Pogba na Rabiot wanakuwa tayari kutumia hiyo space wakipata mpira na kufanya pasi moja ya haraka kwa Mbappe na Griezmann kwa kutumia Counter Attack ya pembeni tena kwa ku switch play .

✍Kama sio offsides mbili bali walikuwa wanafunga magoli kwa plan hiyo ya kushambulia spaces zilizoachwa wazi na mawingback wa Ujerumani ambao walipanda juu .

NOTE

1: Pogba anaufanya mpira kuonekana rahisi sana

2: Mpambano wa Kimmich Vs Hernandez .. nilitamani mechi isiishe , wanafikiana kweli kweli jumlisha kuoneshana ubora 

Post a Comment

0 Comments