AMKA NA BWANA LEO 1
*KESHA LA ASUBUHI*
*ALHAMISI, 01/07/2021*
*MWOKOZI WA HURUMA*
"Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma,ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu. Mpokeeni, basi,katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa. Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake;ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu."
Wafilipi 2:28-30
▶️ Mtume Paulo ambaye alikuwa amepokea mafunuo mengi kutoka kwa Bwana,alikutana na shida kutoka kwa vyanzo anuwai na katikati ya mizozo yake yote na kukatishwa tamaa,hakupoteza imani na ujasiri wake kwa Mungu. Chini ya mafunzo maalumu ya Roho Mtakatifu. Akili yake ilitakaswa,kusafishwa,kuadilishwa, kufanywa takatifu .
Hila za wanadamu na adui dhidi yake zilikuwa njia ya nidhamu na elimu kwake, na anatangaza kwamba kwa hivyo alipata maarifa bora zaidi,kwa sababu alimfanya Bwana Yesu kuwa tegemeo lake. " Ndio bila shaka" anatangaza " Ninahesabu vitu vyote kama hasara kwa ubora wa kumjua Kristo Yesu Bwana wangu( Wafilipi 3:8)...
▶️ Yesu anahisi kila maumivu ya huzuni wanayoyapata wale ambao wamejitoa wakfu kwa huduma yake,na ambao, chini ya shida kubwa wanafanya kazi yake.Hebu tudumu katika Upendo wa Yesu,ili tuwe na ujasiri na imani. Bwana yu hai na anatawala. Kutakuwa na washauri wasio na hekima amabao watajaribu kutuchanganya, Lakini hebu tumtazame Yesu, na kumtumainia kila wakati. Amekuwa msaidizi wetu, na ataendelea kuwa msaidizi wetu.... Wakati mwingine natatizwa Cha kufanya, lakini sitafadhaika.Nimedhamiria kuleta Mwanga wote wa jua maishani mwangu ambao ninaweza.
▶️ Deni ambalo nimepata katika kujaribu kuendeleza kazi ya Mungu wakati mwingine linanitia wasiwasi.Niliingia kwenye deni katika kujaribu kusukuma mbele kazi huko Australia. Uchapishaji wa Tumaini la Vizazi Vyote ulikuwa wa gharama kubwa, na bado nina deni kwa nyumba za Uchapishaji.
▶️Nyumba ninayoishi sasa ililipwa kwa pesa ya kukopwa. Niko tayari kutoa nafasi yangu kama vile nilivyokuwa nikiinunua.Sina mahali pa kukaa katika Ulimwengu huu. Bwana anaposema" Nenda ukaimarishe kazi maeneo mapya," nitakwenda kwa Furaha....
▶️ Uaminifu wangu hautetereki. Sijakatishwa tamaa,Kwa sababu ninaweza kushikilia Mkono wa Kristo.Hebu tuwe wachanagamfu kila wakati, ili wengine wasije kuchukua kutoka kwetu roho ya Kuvunjika moyo.
- Letter 127, July 1,1993,to Elder S.N. Haskell, kwa muda mrefu akiwa mtenda kazi mwenza wa Ellen White's, Wakati akifanya uinjilisti jijini.
Post a Comment