*KIZOTA NET-EVENT 2021, SHANGWE KATIKA NJIA YAKE.*
KAYA NA FAMILIA.
TRH. 18/06/2021.
DEVOTHA SHIMBE.
*SOMO: MAMBO YA PESA KATIKA NDOA.*
Miongoni mwa talaka nyingi leo zinatokana na masuala ya pesa. Hivyo somo hili leo litatuelekeza kuelewa vyema juu ya suala zima la pesa katika ndoa.
Pesa inaweza kukusaidia kupata mahitaji yako lakini isikupe furaha katika ndoa yako.
Wanawake wengi hupenda kuishi na wanaume wenye pesa pasipo wao kufanya kazi, ukilinganisha na wale wana pesa za kuungaunga.
Wanawake wenye kiwango kikubwa cha pesa katika ndoa husababisha wanaume wengi kutokuwa na ujasiri katika suala zima la pesa wakidhani watatawaliwa. Hivyo hii huweza kuleta changamoto katika ndoa.
Mabishano kuhusu pesa husababisha talaka.
Matumizi ya pesa katika ndoa pia husababisha migogoro katika ndoa.
Watu wanavutiwa na wenzi wenye uwezo mkubwa wa kupangilia bajeti katika vitu vinavyohitaji pesa pasipo kutapanya pesa.
Hizo ni kutoka katika tafiti mbalimbali ulimwenguni.
Njia za kusimamia pesa:
Kila mtu ana njia yake katika namna ya kusimamia pesa.
Njia mojawapo ni hizi:
1. Hutegemea kipato cha wanandoa.
2. Mitazamo ya wanandoa. Kwamba kikitumika kifanyike kwa namna gani.
3. Utamaduni.
4. Tabia kuhusiana na matumizi ya pesa.
5. Vipaumbele vya kila mmoja. Je, ni biashara au uwekezaji. Hii nayo ni njia sahihi.
Aina za wanandoa na pesa.
1. Wanandoa wanaounganisha vipato vyao.
2. Hakikisha mioyo yenu wote ina amani na kila mmoja ana uwezo wa kuzitumia bila ubinafsi.
3. Makubaliano namna ya kuunganisha kipato chao. Huyu anatoa asilimia ngapi na mwingine asilimia ngapi.
4. Wanandoa wasiounganisha kipato kabisa. Hakuna anayefahamu kipato cha mwenzake. Kila mtu yuko kivyake tu.
5. Wanandoa wanaoshirikiana majukumu pamoja kwa kuzingatia kipato chao. Matumizi yenu yasizidi kipato chenu.
6. Aina za wanandoa wanaogawana majukumu ya kifamilia. Mfano mmoja anasomesha, mwingine ujenzi nk.
7. Wanandoa ambao Mmoja anamlipa mwenzi posho katika ndoa.
8. Wanandoa wanaoishi kwa kipato kimoja.
Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:24
Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
Mwanzo 2:25
*MUNGU ATUBARIKI SOTE.*
chirongemagai74@gmail.com
🙏🙏🙏🙏
0 Comments