Advertisement

Responsive Advertisement

USITOE MIMBA

*YAWEZEKENA IKAWA CHUNGU KWAKO ILA IMEZE TU ITAKUSAIDIA.*
*LEO NAZUNGUMZA NA MABINTI WOTE WANAOBEBA UJAUZITO NA BADAYE KUUTOA/ KUTUPA KIUMBE KISICHOKUWA NA HATIA.*
*Usiue.*
Kutoka 20 :13.
*Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.*
2 Timotheo 2:22
Karne hii tuliyopo na kizazi hiki tunaendelea kuona mambo mbalimbali yakitokea yanayotikisa ulimwengu. Hatuogopi kwa sababu yalishasemwa katika Neno la Mungu tangu mwanzo.
Inasikitisha leo tunakutana na mabinti wazuri, warembo sana wenye maumbo ya kila aina lakini wana roho za UUWAJI, UKATILI, UNYAMA na kila aina ya uovu. Si walio wakristo au wasio wakristo wote wapo kundi moja. 
Na ndiyo maana utakuta mauaji katika NDOA, na hii ndiyo inapelekea watu kusema ndoa ni ndoano jambo ambalo si kweli. NDOA NI TAKATIFU INATEGEMEA ULIINGIA NA NANI? KAMA NI MUNGU ITAKUWA NJEMA, KAMA NI SHETANI UTALIA NA KUSAGA MENO.
Unapoona wanandoa wamechomana visu, au mmoja amemuua mwenzake utagundua kuwa ukatili haujaanza leo, ulianza zamani mno. Eti utasikia mwanamke amemchoma kisu mume wake na amefariki huyu kuna sehemu alipoanzia ukatili.
*Binti kwa tamaa yako mwenyewe unaondoka kwenu au unapoishi iwe ni chuoni, nyumbani, shuleni nk, unamfata kijana wa kiume kwa makubaliano yenu wenyewe unaenda kwa sababu tu ulishaambiwa NAKUPENDA. Lakini unapoenda unasahau matokeo yatakayojili baada ya hiyo VISITATION uliyoifanya pale kwa huyo mwanaume.*
Ulienda mwenyewe mkafanya uzinifu mkiwa wawili pale chumbani matokeo yake ukatoka na UJAUZITO. Swali la kujiuliza kwanini baada ya kuubeba na kukua unaua huyo mtoto? Kwanini unautoa huo ujauzito wakati hayo ndiyo ulikuwa unayatafuta? Na ulipomwambia kijana upendo ukatoweka. Je, kati ya nyinyi na hicho kiumbe nani mwenye kosa? Hamjui kama mlifanya jambo linaloangamiza nafsi zenu?
*MABINTI MTUBU UKWELI NI KWAMBA WEWE PAMOJA NA ALIYEKUPA UJAUZITO MTAKUWA NA CHA KUJIBU SIKU YA HUKUMU TUBUNI LEO.*
HIVI KWELI UNAZAA MTOTO UNAMTUPA, UNABEBA UJAUZITO UNAUTOA ALAFU NA WEWE UNATEMBEA MTAANI UNAJIONA NI BINTI SAFI KUMBE NI MAMA WA MAREHEMU TAYARI, BINTI YEYOTE ULIYEFANYA HAYO FAHAMU KUWA WEWE NI MAMA WA MAREHEMU TU, HATA UNGEJIREMBA UKANG'AA KWA NAMNA GANI. BIDHAA FEKI NI FEKI TU NA ORIJINO NI ORIJINO. NA NDIYO MAANA WENGI HAWAOLEWI KWA SABABU YA LAANI HII NA MATOKEO YAKE NI KUHARIBU NDOA ZA WATU KWA KUWABEBEA WAUME WA WANAWAKE WENZAO, ACHENI, VINGINEVYO RUDI KWA MUMEO ALIYEKUPA UJAUZITO BADAYE UKAUTOA MAANA NDIYE MLIPATANA HIVYO KAPATANENI TENA SASA MWOANE. NA WEWE MWANAUME TAMBUA KUWA WEWE NI BABA WA MAREHEMU MAANA ILE NI DAMU YAKO TENA IKO MIKONONI MWAKO HATA LEO.
Wapo akina mama wanaoshiriki huu UOVU na mabinti zao, mama anajua binti wake ana ujauzito eti kwa kulinda heshima yeye ndiye anafanya michakato yote kuhakikisha ujauzito huo unatolewa tena kwa siri ili baba asijue. Lakini wengi huwa wanaumbuka pindi binti anapokuwa na hali mbaya, na wengine wamefia mikononi mwa mama zao. AKINA MAMA WA JINSI HII MKATUBU PIA. NA HII KWA MAANA NYINGINE NI KANA KWAMBA MAMA NA BINTI YAKE WOTE WALIKUBALI KUFANYA UZINZI NA HIVYO WANAKUBALIANA KUUWA WOTE.
*NA YAWEZEKANA KABISA UKIOA MWANAMKE ALIYEWAHI KUTOA UJAUZITO AU ALIYEJIFUNGUA MTOTO AKAMTUPA, JUA TU UMEOA KATILI NA MUWAJI, NDIYO WALE WAKIWA KWENYE NDOA WANACHOMA WATOTO WAO MOTO, WADADA WA KAZI WANATESWA HOVYO HUYO ALIANZA UKATILI ZAMANI. HEBU JIULIZE KAMA HAKUANZA ZAMANI HUO UNYAMA NA UKATILI ALIUTOA WAPI?* IKIWA MWANAO ULIMUUWA TOKA TUMBONI UTATHAMINI WA WENGINE? LA! HATA AKINABABA KATILI NI WALE WALIOKUWA WANAWAPA UJAUZITO MABINTI NA BADAYE WANAWASHURUTISHA KUUTOA. HAWA NDIO AKINA BABA KATILI WALIOPO LEO KWAO KUUWA NI JAMBO LA KAWAIDA KWANI HAJAANZA LEO.
WAKO MABINTI KULE VYUONI HII NDIYO KAZI YAO YAANI HATA ANACHOKISOMA KINAMSHUHUDIA KWAMBA NI NAMNA GANI ALIVYO MPUMBAVU NA USOMI WAKE NI BURE. BINTI MSOMI HAWEZI KUWA KATILI NA HIVYO WEWE UKO ULIKO UNASOMA TU NAMNA YA KUWA KATILI WA BADAYE. TUBUNI.
KIJANA IKIWA ULISHIRIKI NGONO NA BINTI UKAMWACHA AKATO ULE UJAUZITO USIFIKIRI KUTEMBEA MTAANI UKIWA NADHIFU UMESHINDA, BADO NA WEWE LAANA INAKULILIA MLANGONI. ULIMPA UJAUZITO UKAUKATAA NA WEWE NI MUUWAJI NENDENI MKATUBU WOTE LASIVYO WOTE HAYUPO ALIYE SALAMA KATI YENU. HATA KAMA NA WEWE ULISHIRIKI KUUTOA UKATOA NA PESA TAMBUA TU UTAKUWA NA CHA KUJIBU SIKU YA HUKUMU TAMAA NI MBAYA, DHAMBI NI MBAYA NA HIVYO YESU ANAWAITA LEO MTUBU.
*LEO WAPO WANAWAKE NI WAGUMBA, LAKINI WENGINE WALIPENDA WENYEWE KUWA WAGUMBA KWANI SIKU ALIPOTOA UJAUZITO ALITO KILA KITU KATIKA KIZAZI NA LEO HAWEZI TENA KUZAA, WAPO WALIOJIFUNGUA WAKATUPA WATOTO KUMBE NDIYE ALIKUWA HUYOHUYO BASI.* JITAFAKARI.
*HERI UWE SINGLE MOTHER AMBAYE ULIONA THAMANI YA MWANAO UKAMZAA, KULIKO KUWA SINGLE GIRL ALIYE MASHUHURI WA KUTOA KILA AINA YA UJAUZITO NA ANATEMBEA BILA KUJUA KUWA NI MAMA WA MAREMU, WAKATI WA MUNGU UKIFIKA UTALIA NA KUSAGA MENO, KWANI WAPO WANAOTOA UJAUZITO ZAIDI YA MOJA LAKINI WAPO SALAMA TU. WAKATI WA MUNGU UKIFIKA UTALIA, HERI UACHE LEO UMRUDIE BWANA.*
*VIJANA WA KIUME ACHENI KUWALAGHAI MABINTI NA NYIE MABINTI TULIENI KWA YESU MTAKUWA SALAMA, MSIPOKUBALI NA KUTII MTAENDELEA KUHARIBIWA NA KUISHIA MAJUTO MAKUBWA, BINTI ALIYEJIWEKA WAKFU KWA BWANA HAKUNA KIJANA MWOVU ANAYEWEZA KUMSOGELEA.*
DHAMBI NI TAMU UNAPOITENDA LAKINI MWISHO WAKE NI UCHUNGU NA MAJONZI TELE. ACHA DHAMBI YA TAMAA.
MWISHO MUNGU ATUTIE NGUVU KUTAMBUA KUWA YESU ALITUFIA WOTE MSALABANI NA LEO ANATUITA TWENDE KWAKE NA MIZIGO YETU YA UOVU, MAKOSA, NA DHAMBI ATUSAFISHE TUWE SAFI, MPOKEE LEO.
🙏🙏🙏🙏

Post a Comment

0 Comments