Advertisement

Responsive Advertisement

ULEGA AAGIZA KUTAFUTA SULUHU YA OKOSEFU WA MALIGHAFI

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (Mb) amewaelekeza viongozi wa viwanda vya kuchakata samaki Mkoani Mwanza kukaa na maafisa kutoka katika wizara hiyo kutafuta suluhu ya ukosefu wa malighafi ya kutosha katika viwanda vyao ili viweze kufanya kazi kwa kadri ambavyo vinatarajiwa.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo jana (23.05.2021) wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo kwa kutembelea viwanda vya kuchakata minofu ya samaki vya Tanzania Fish Processor na Victoria Perch Limited baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa viwanda juu ya ukosefu wa malighafi ya samaki aina ya sangara.

Post a Comment

0 Comments