Advertisement

Responsive Advertisement

SADC YAITISHA KIKAO CHA DHARURA

Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC imeitisha mkutano wa dharura wa utatu wa Jumuiya hiyo wenye lengo la kujadili mapendekezo ya Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Afya kuhusu hali ya ugonjwa wa COVID – 19.

Katika Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Joseph Edward Sokoine ambapo takwimu zinaonesha kupungua kwa maambukizi na vifo katika Bara hilo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi May 2021 Bara la Afrika limeripotiwa kuwa na visa vipya arobaini na mbili elfu ambapo vifo vipya ni Zaidi ya elfu moja na hivyo kushauri kuwa mikutano ya Jumuiya hiyo katika ngazi mbalimbali iendelee kufanyika kwa mseto wa ana kwa ana au kwa njia ya mtandao.

Post a Comment

0 Comments