Mpira wa miguu ni mchezo katili sana, unafurahisha kwa wakati huohuo unahuzunisha.
Matokeo waliyopata Simba dhidi ya Kaizer ni ushahidi wa hilo. Fikiria jasho lote lile walilomwaga halafu bado wametoka.
Unapoitazama Simba, unajiuliza ni timu hiihii ilifungwa nne Afrika Kusini?? Huwezi kuamini.
Kitu kimoja cha kuwapongeza Simba kabla ya kila kitu ni Roho ya UJASIRI NA MAPAMBANO waliyokua nayo.
Si rahisi kuwa nyuma mabao manne halafu bado ukafanikiwa kurudi mechi ya pili na 'MENTALITY' ile ya Simba. Kwa ule Moyo nawapigia saluti.
Nimeipenda sana Approach ya Didier Gomes lakini kuchagua kucheza krosi za juu dhidi ya mabeki kama wale wa Kazier ni kutishia kumnyonga samaki kwa maji.
Kitu kitakachowaumiza zaidi Simba, ni kutumia nafasi chache kati ya nyingi walizozitengeneza, haswa mwisho wa siku unapokosa bao moja tu.
Siku nikikutana na Didier Gomes, nitamuuliza kuhusu ubora wa Chris Mugalu mbele ya Meddie Kagere. Hata dakika kumi tu Kagere angezishindwa??
Again! Simba wamepambana sana. Hata kama wameondoshwa wameonesha ukubwa wao. Ni dhahiri sasa kila timu Afrika inajua Tanzania kuna klabu inaitwa Simba.
0 Comments