Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewataka wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha Magari ya uzoaji taka yaliyotolewa kupitia Mradi wa Uboreshaji na Uendelezaji Jji la Dar es Salaam (DMDP) yanatumika kikamilifu kama ilivyokusudiwa ili kuongeza ufanisi katika uzoaji taka.
Prof. Shemdoe ameyasema hayo Alhamisi tarehe 13 machi, 2021 alipofanya ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa DMDP katika Jiji la Dar es Salaam (zamani Manispaa ya Ilala) ambapo hakuridhishwa na baadhi ya Manispaa za Dar es Salaam kutoanza kutumia magari hayo licha ya kuwa na changamoto ya uzoaji taka.
“Nimefurahishwa na kazi ya ununuzi wa magari pamoja vifaa vyake vya kuzolea taka iliyofanywa kupitia mradi huu, lakini nimepata maelezo kuwa kuna baadhi ya Halmashari bado hazijaanza kutumia magari haya. Sasa niwaambie wale ambao hawatumii magari haya tunaweza kuja na mpango wa kuyachukua na kuyagawa kwa Halmashauri zenye Uhitaji,”alisema Prof. Shemdoe.
Aidha aliwaaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Dar es Salaam kuja na mpango mahususi wa kuonesha jinsi magari hayo yaliyotolewa yatakavyotumika kikamilifu na kuhakikisha yote yanafanya kazi iliyokusudiwa na Mkoa unakuwa safi.
“Viongozi wenzangu Wakurukenzi wa mamlaka hizi, leo ni tarehe 13 May, 2021, mpaka tarehe 20 May, 2021 niletewe mpango wa namna gani magari haya yanaweza kutumika kwa shughuli iliyokusudiwa, la sivyo nitayatoa kwa Halmashauri zingine ambazo zinaweza kuyatumia,” alisema Prof. Shemdoe.
Kupitia mradi huo wa DMDP takribani magari 20 yalitolewa ambapo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilipewa magari matano (5), Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni magari matano (5), Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo magari mawili (2), Halmashauri ya Manispaa ya Temeke magari saba (7) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni magari mawili (2).
Kwa upande mwingine Prof. Shemdoe alifurahisha na ujenzi unaoendelea wa madaraja makubwa mawili katika maeneoya Ulongoni B na Zimbilli kata ya Kinyerezi.
0 Comments