Advertisement

Responsive Advertisement

PART 1 NA MALISA GJ

Mama ametupa zawadi nzuri ya Eid. Huu ni ushahidi kuwa Sabaya ameumiza watu wengi ndio maana maamuzi ya kumfurusha yamepokelewa kwa furaha kubwa na nchi nzima.

Jambo la muhimu zaidi mama hajaishia kumfurusha tu bali ameagiza ufanyike uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ili afikishwe mahakamani. Kwahiyo sasa hivi Sabaya ni mtuhumiwa. Muda wowote tutamuona nyuma ya karandinga.

Sabaya ana tuhuma mbalimbali (lukuki) kama taarifa ya Ikulu ilivyoeleza. Anatuhumiwa kupora, kunyanyasa na kutumia madaraka yake vibaya. Tuhuma hizi zimekuwepo tangu enzi za mwendazake lakini amekua akilindwa.

Yeye mwenyewe amewahi kujitapa kuwa hakuna anayeweza kumpa order isipokua mwendazake pekee. Alimdharau hadi RC wake. Ndio maana mama Mghwira alipomwambia aache kutumia mabavu alimcheka kwa dharau. Mwaka 2019 PM alifanya ziara K'njaro wafanyabiashara wakamueleza jinsi Sabaya anavyowanyanyasa, lakini hakuchukua hatua yoyote. Akasema atayafikisha kwa mamlaka yake ya uteuzi.

Lakini hakuna chochote Sabaya alichofanywa. Badala yake alizidi kuwa kiburi kuliko mwanzo. Wale wafanyabiashara "waliomchongea" kwa PM walipata joto ya jiwe. Na PM hakuwa na chochote cha kumfanya. Hatimaye leo mama amevunja kisiki kilichowashinda maksai.

Sabaya anatuhumiwa kutumia mabavu kupora fedha kwa wafanyabiashara mbalimbali. Mmoja wao ni Cuthbert Swai mmiliki wa Asante Tours na Hoteli ya kitalii ya Weruweru.

Cuthbert anadai mwaka 2018 Sabaya alitaka ampe 10M otherwise atampa kesi ya uhujumu uchumi. Kwa kuhofia jela akampa. Baadae akataka tena 10M, akamwambia hana. Baada ya vitisho vya mara kwa mara, wafanyabiashara wenzake wakamwambia mpe tu, usicheze na mjinga atakutoboa jicho. Akampa kishingo upande.

Baada ya miezi michache Sabaya akamwambia kuna "special mission" amepewa hivyo inatakiwa pesa nyingi kuitekeleza. Kwahiyo wafanyabiashara wanatakiwa wachangie. Akamtaka Cathbert atoe 15M. Cuthbert akamwambia biashara ya utalii imeyumba hivyo hawezi kupata fedha hizo.

Na hapo akatangaza uhasama na Cathbert. Akaenda kwenye mashamba yake huko Rundugai akasema alidhulumu wanakijiji. Akatengeneza wazee feki waliojifanya wamedhulumiwa, halafu akatangaza kuyataifisha.

Post a Comment

0 Comments