Hakuishia hapo akavamia hoteli ya kitalii ya Weruweru inayomilikiwa na Cathbert. Siku hiyo Nandy alikua na show Arusha, akalala Weruweru. Usiku saa 9 Sabaya akavamia akiwa na kikosi cha watu 6 wenye silaha. Akalazimisha aoneshwe chumba cha Nandy, mhudumu aliyekua mapokezi akakataa. Sabaya akampiga sana. Walinzi walipotoka nao wakapigwa na mabaunsa wa Sabaya.
Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV camera but who cares? Pamoja na video hiyo kusambaa lakini hakupewa hata onyo. Utamwambia nini mtoto pendwa wa mwendazake? Aliwahi kujitapa kuwa yeye ndiye DC pekee anayeweza kumpigia simu mwendazake usiku wa manane na akapokea.
Akaendelea kuvuruga biashara mbalimbali za Cathbert na kuagiza TRA wafreeze baadhi ya akaunti zake. Hali ikawa ngumu hadi mali za kampuni ya Asante Tours zikapigwa mnada. Akavuruga shamba la wanyama (zoo) la Cuthbert maeneo ya Maili sita. Akaharibu mizinga 200 ya nyuki kwenye shamba la Cathbert kwa madai hana kibali cha maliasili cha kufuga nyuki.
Baada ya hapo Cuthbert anadai Sabaya alitishia kumuua. Ikamlazimu kukimbilia ziwa Jipe mpakani mwa Kenya akaishi huko. Zaidi ya watu 300 waliokua wameajiriwa kwenye biashara zake mbalimbali wakapoteza ajira kwa sababu ya Sabaya. Just imagine.
Lakini hakuishia kwa Cuthbert, akaendelea kufanya ukatili kwa watu wengine. September 2020 alivamia hoteli ya Protea Aishi iliyopo Machame, inayomilikiwa na Freeman Mbowe. Hotelini hapo kulikua na wageni kutoka nje ya nchi wanaopanda mlima Kilimanjaro.
Sabaya akawakamata na kudai wamekuja kusaidia Chadema kwenye uchaguzi. Wakatolewa hotelini usiku wa manane na night dress kupelekwa kituo cha Polisi Bomang'ombe. Wakahojiwa na kuachiwa, lakini wamesababishiwa usumbufu, na wameweka doa kwenye sekta yetu ya utalii. Kumbuka tunatumia fedha nyingi kutangaza utalii, halafu mtu mmoja anawadhalilisha kwa mihemko tu.
Siku ya uchaguzi (October 25) alivamia tena Aishi hotel akiwa na magari yenye namba za UN. Wakawapiga walinzi na kukamata baadhi ya mawakala wa Chadema waliokua hapo. Wakawatia matambara mdomoni na kuwapiga sana kabla ya kwenda kuwatelekeza maeneo ya Sanya stesheni usiku huo.
0 Comments