“Huu mradi wa Bomba la Mafuta ni sehemu ya miundombinu kwa ajili ya kuleta ajira kwenye zile sekta za (Elimu, Usafiri, Afya na Kifedha), ila ni wasihi Watanzania na Waganda wasijisahau sana kwenye hii sekta ya mafuta wakasahau sekta nyingine kama kilimo.
Ninafuraha kwamba Serikali ya Tanzania imekubali kusaini mkataba wa Uenyeji wa mradi pamoja na ushiriki wake kwenye ujenzi wa mradi wa Bomba la mafuta.
Bomba hili la mafuta ni muhimu sana kwenye Ukanda mzima wa Afrika wa Mashariki, najua hapa Tanzania na Msumbiji mna gesi na sisi Uganda tunahitaji gesi hasa kwenye viwanda vya chuma.” Rais wa Uganda Mhe Yoweri Museveni.
0 Comments