EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

Hio picha ni logo ya biashara niliowahi kufanya.

Basi lile wazo lilikuwa hivi niandike waraka ambao utaelezea maisha yangu na nini nataka kufanya na changamoto iliopo ili watanzania wanichangie niweze kununua bajaji yangu ili kutatua changamoto ya usafiri kweli nikaliandaa hilo andiko na huyo rafiki yangu na baadae tukalirusha mitandaoni facebook, na magroup mbali ya watsaap kiukweli watu wengi liliwafikia nikaanza kupokea michango. 

Nikajiongeza nikachukua jiko la gas na baadhi ya materials ya kuanza kufanya biashara huku nakusanya michango huku nikawa nimeanza kutangaza biashara yangu nikaajiri chef na mtu wa wa kufanya delivery kwa kutumia daladala au boda boda. 

Michango ikawa inaenda vizuri hapo target ni kukusanya milion 7 nipate bajaji mpya. 

Zile pesa nilizokuwa nakusanya nikazitoa kwenye simu kama milion 3 hivi nikasema nizihifadhi ili nikipata time niende kuziweka Bank. 

Wakati napata hela ya chakula kuuza nikasema ngoja nianzishe biashara nyingine ya kuuza vitenge wax basi nikatafuta connection kigoma huko nikawa nachukua mzigo then nauza Dar wazo la kutafuta kazi likaisha basi ikaenda hivoo kwa muda sasa siku moja ilikuwa jumatatu hivi.

Tumeamka asubuhi dada yangu idda akawa ameenda kazini akanipigia simu mdogo wangu naomba nikopeshe kiasi cha pesa mpe shemeji yako nikirudi jioni ntakurudishia nikamwabia sawa nikasema ngoja niende kuchukua ndani nilikozificha zile pesa ili nimpatie kwenda kuzitazama hakuna pesa mmh nikastuka sana nikamuliza kaka wa kazi alikuwepo akasema hafahamu aisee nilihisi kuchanganyikiwaaa niliona presha kama inashuka nikakosa nguvuu kabisaaa nikampigia dada simu kumweleza kuwa pesa nilizificha sehemu hazipo dada nae akawa haelewiii kiukweli nilivunjika moyoo sanaaa nikaumia mnooo nikajiuliza nani amechukua hela yangu maana nilificha kabatini na ndio nilikuwa nataka kuipeleka bank sikupata majibu Nilipaniki sana dada akarudi home tukaanza kujiuliza nani alikuja nyumbani weekend maana ijumaa zilikuwepo jmosi tulienda harusini jpili tukashinda tu nyumbani na jmatatu ndio hazipo tukataka kujua nani alikuja tukaambiwa kuna ndugu walikuja wawili tukawapigia simu waje home tuwaulize wakaja.

No comments