• HOME
  • BREAKING NEWS
  • TAMTHILIA
  • MICHEZO
  • MATANGAZO
  • CONTACT US

BINAGO BLOG

  • Home
  • Home / Habari / EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

    EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

    Bisaya Raphael May 11, 2021 Habari
    Walivyokuja wale ndugu tukawauliza wakasema hawahusiki nilikosa matumaini kwa kweli nikasema yani mtu unapambana ili utoke kimaisha halafuu anatokeaa mpuuzi mmoja ananirudisha nyuma nikamwambia dada hii sikubali ita shehe asome alibadiriibna ambae amehusika basi akutane na balaa lolote huko. 

    Kweli tukafanya hivo lkn moyoni sina Amani nimekosa pozi la kuendelea na biashara tena. 

    Ila baadae nikakaa nikamuliza Mungu kwanini unaruhusu haya au una mipango mikubwa zaidi ya hii ??? Nikamwachia Mungu nikasema nifanyeje sasa sikuwahi kuwaambia hili marafiki walionichangia ila leo nawaambia na naomba MNISAMEHE SANA SANAA. 

    Basi nikasema kilichobaki nikuomba kazi tu serikalini niajiriwe nifanye mambo mengine nilikuwa na balance kidogo nikasema hii pesa ninunue TV na ving'amuzi nianze kuonesha mpira mtaani nikusanye hizo mia tano mis tano na buku buku nikafanya hivo na nikapata sehemu hapo mtaani huku nikitafuta kazi basi Mungu si Athumani zikatoka nafasi za kazi na kuomba hio ni 2017 nikaitwa kwenye interview ya kuandika nakumbuka ilikuwa kule kigamboni chuo cha nyerere nikakuta watu ni wengiii mno kama watu 2000,tukafanya zile interview lkn moyoni najisemea mmh hapa hamna kitu. 

    Tukarudi nyumbani baada ya siku 3 nikapokea meseji kuwa natakiwa kwenye Oral interview posta maktaba house nikaenda nikaambiwa tupo 54 basi nikakutana na Jopo nikapigwa maswali pale ya kingereza daah nikamaliza nikaambiwa utapewa majibu yako baada ya miezi kupita nikawa nishajikatia tamaa nikasema hapa mjini kumeshanishinda nirudi tu kijijini kupumzika na mama huku naiwaza pesa yangu ilioibiwa. 

    Sasa baadae ilikuwa december 2018 mwanzoni nikatumiwa meseji na rafiki yangu oyaa nimeona jina lako hongera kwa kupata kazi..mmh nikamwambia unazinguaa akanitumia link niangalie kila nikiangalia sioni jina nikaacha kuangalia kuna mtu mwingine akanitext hongera kwa kupata kazi nikamjibu mbona mm sioni. 

    Sasa ndio kutulia nikaona jina ila hilo jina la mwisho halikuwa langu nikasema sio mimi huyu,nikamuonesha idda akaniambia hili jina wamekosea ni ww kesho nenda kawaulize nikaanza kumgomea maana nahisi ni kujichosha tu,asubuhi idda akaniamsha ili niende nikaamka kivivu vivu ila SHETANI HUYU NI MSHENZII.

    Related Posts

    Habari

    Post a Comment

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    KWA SHEREHE NA SEMINA KARIBU UKUMBI WA LAKE TANGANYIKA, NZEGA-TABORA

    FOOTBALL STORIES

    Follow us

    • Like on Facebook
    • Follow on Twitter
    • Follow on Instagram
    • Subscribe on Youtube

    Popular Posts

    • kusuka na unyoaji katika Biblia
      kusuka na unyoaji katika Biblia
       KAMA MUNGU ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAWAKE ! NDIVYO ALIVYOKWISHA KUWAONYA WANAUME PIA. BWANA YESU asifiwe!😅 Maranatha!😅🙏🏻 N...
    • Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      Je kutoa Mahari ni sawa ktk biblia?
      *https://youtu.be/-P4s8sVq31o* 🤔🤔🤔🤔🤔 *JE NI HALALI KWA MKRISTO KULIPA MAHARI ILI AOE?????* 🤔🤔🤔🤔🤔 . . . Hebu tutazame k...
    • HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      HII NDIO MISINGI YA KANISA LA WASABATO DUNIANI
      KANISA LA #SDA LINA MISINGI 28 AMBAYO NI 1.Neno la Mungu 2.Utatu mtakatifu 3.Mungu baba 4.Mungu mwana 5.Roho mtakatifu 6.Uumbaji...

    Labels

    Habari MICHEZO Live injili Tamthilia Kesha la Asubuhi BREAKING NEWS magazeti Matangazo Covid19 Mastaa Viongozi today's quote Lesoni leo Wimbo wa Leo barikiwa Je Wajua? KULFI Bongo Movies Stories TETESI ZA USAJILI

    Facebook

    Created By SoraTemplates | Distributed By Gooyaabi Templates