EPSODE 5 NA KANKWI WA KANKWI

Tuendelee basi Mungu akajalia nikamaliza miaka yangu 3 pale udsm vizuri tu nikarudi zangu mtaani sasa kupambana na maisha mengine huku nikisubiria matokeo ya mwisho nijue je Joho litavaliwa au ndio mambo ya SUP basi wakati niko mtaani nikawa najichanganya na shughuli za kijamii ndipo nilipokutana na SMILE VOLUNTEERS @smilevolunteers under the founder Kelvin Mwita @kelvinmwita huyu ndugu alikuja na hio idea akiwa chuo cha muccobs lecturer na kuamua kuwaunganisha vijana wote vyuoni hapo na hata nje ya chuo na nia ni kusaidia jamii kwa watu wenye uhitaji au makundi maalumu kwa kujichangisha kidogo kidogo ili kupata fedha kununua mahitaji ya hayo makundi na kwenda kuwasaidia sasa smile volunteers ikawa na wanachama wengii mpaka Dar na morogoro sasa mm ndio nika join branch ya Dar na nikawa najitolea humo nikawa mmoja wa viongozi wake basi tukawa kweli tunajitolea hivo hivo sisi wenywe na kwenda kusaidia makundi maalumu. 

Baadae matokeo ya chuo yakatoka namshukuru Mungu matokeo yangu yalikuwa mazuri sanaaaa ikawa sasa nina mhaho wa graduation. 

Wiki moja kbl ya tarehe ya graduation nikawa nikilala naota ndoto za ajabu ajabu sanaa nikawa nazitafakari mno mara niote joho limepotea mara kofia ile imeungua yani ndoto ambazo zilikuwa zinanipa picha ya kuwa lbd graduation sitoifanya huwezi amini wiki nzima naota nikawa sijamwambia hata idda sasa ilipofika siku yenyewe sikutaka hata sijui niende saloon nilimwita kinyozi nyumbani nikaoga nikamaliza nikavaa ndio nikamhadithia dada angu idda akaniambia tu usijali utakuwa sawa tukasali pale then nikamuita dereva tax nikamwambia nipeleke mlimani city ila nikampa sharti unipeleke mdogo mdogo hadi eneo la tukio na nikifika nipeleke hadi ndani tulivyofika nikamshukuru Mungu nikaingia ndani ya ukumbi nikatulia tuliiii sikutaka hata kutoka nje kupiga sijui selfiee mpaka shughuli ilipo anza na mpaka ikaisha sasa nikawa najua baada ya hapa ni nyumbani kusherekea na familia yangu na marafiki baadhi kumbe haikuwa hivo kumbe kulikuwa na kamatiii maalumu ilioundwa tangu mwezi mzima kwa ajili ya party yangu walikuwa marafiki baadhi na familia yangu ( iddas family ) na mama yangu.

No comments