CRISTIANO RONALDO NA PENALTI BORA YA MAISHA YAKE
NA FARHANJR;
Nikiwa bado natetemeka kwa baridi kali sana kutokana na mvua niliyonyeshewa njiani kwa mguu kutoka shuleni mpaka kwenye banda la mpira, Mei 28 usiku wa mvua 2016 pale Tukuyu Mbeya, kutoka Igogwe mpaka Kiwira
Dakika 120 zimeshakatika, inaelekea saa saba usiku, tayari ni penalti 4-3, Luca Vasquez alikuwa wa kwanza, akafata Marcelo Viera, akaja Gareth Bale na El Capitano Sergio Ramos, tena zote zikienda upande wa kushoto wa Jan Oblak, wahafidhina Madridista wanasubiri maajabu ya mtu mmoja tu
Captain Sergio Ramos anampiga mgongoni Cristiano Ronaldo kisha anamwambia "Dale Cristiano" yani nenda kamalize, wakati Ronaldo anapiga zile hatua zake nawaza sehemu ngumu zaidi alizotupitisha, namkumbuka Ronaldo wa kamba tatu dhidi ya Wolfsburg, alitupitisha pia kwa Warumi wa Roma
Wakati namuwaza Cristiano akiwa anapiga hatua, wachezaji kama wanne wa Real Madrid walikumbatiana na kulipa mgongo lango, nilimuona Pepe wa Ureno kainama chini kabisa, Danilo wa Brazil kaziba macho, Swahiba wake Marcelo hataki kutazama, nikamuona Isco anasali kabisa, ila Ramos katulia anamtazama kijana wake
Wakati Cristiano anauchukua mpira na kuubusu nilimuona golikipa Kaylor Antonio Navas Gamboa akinyoosha mikono juu kuiita miungu ya Costa Rica ile Arenal kutoka Cordillera kwenye milima ya Chirripo, bila shaka ilishuka kuleta baraka ya penati ile
Nilimuona mtoto mmoja jukwaani, anapiga ishara ya msalaba na kama sikosei alikumbuka neno la Bikira Maria alipowatokea watoto wa Fatima wale Lucia, Francis na Yasinta, wasali rozari ili kupata baraka na maombezi, bila shaka baraka zile za Bikira Maria zilishuka kwa Cristiano
Namsikia Mtangazaji Andres Cantor akitangaza kwa hisia kali sana "Vamos Cristiano" anairudia kwa zaidi ya dakika moja, kisha Ronaldo anasimama vyema na viatu vyake vya NIKE Mercurial Vapor Superfly, anatembea hatua kadhaa kisha kuupeleka mpira upande wa kushoto, ni chuma
Ni kombe la 11 kwa Real Madrid lakini kombe la tatu kwa Cristiano Ronaldo, Perez jukwaani ananyanyua mikono juu, ni mwezi kama huu miaka minne iliopita

Post a Comment