Watu wenye silaha wamevamia Chuo Kikuu katika Jimbo la Kaduma, Nigeria, na kuwateka wanafunzi.
Hicho ni Chuo Kikuu cha Greenfield kilichoanzishwa miaka mitatu iliyopita na haikufahamika mara moja idadi ya wanafunzi waliotekwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu wenye silaha walivamia chuo hicho usiku wa jana na kuanza kushambulia kwa risasi.
Katika siku za hivi karibuni, Jimbo la Kaduna limejikuta kwenye majanga ya aina hii kwani mwanzoni mwaka huu wanafunzi 39 walichukuliwa na watu wanaohusishwa na Kundi la Boko Haram.
0 Comments