Advertisement

Responsive Advertisement

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, GERSON MSIGWA LEO APRIL 21 AMEFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Aprili 21, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo zilizopo jijini Dodoma.

Pamoja na ushirikiano baina ya pande mbili hizo wamewakumbusha wanahabari kuwa kipindi cha mpito kinachowataka kuwa na Diploma kinaishia Desemba 31, mwaka huu.

Hata hivyo Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewatoa hofu wanahabari kuwa wasichukulie hasi Kanuni ya Sheria hiyo kwakua ina malengo chanya kwa taalum hiyo nchini.

“Mtu anayelima Muhogo, hawezi kulima tu bila kufuata kanuni bora za ukulima wa muhogo’ hivyo itampasa kupata elimu ya namna bora ya kulima ili kupata ama kuongeza tija," amesema Msigwa.

Post a Comment

0 Comments