Wananchi wa maeneo mbalimbali ambao hawana umeme katika kata ya Nyamagana jijini Mwanza wameombwa kutumia nishati ya jua ili waweze kupata mwanga na kuacha kutumia taa zinazotumia mafuta ya taa, na mishumaa ili kuepuka majanga ya moto.
Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Nyamagana (CCM), Bhiku Kotecha wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la ofisi ya kampuni ya D.LIGHT lililofunguliwa Mkoani hapa.
Alisema ili kuepuka majanga ya moto kila mzazi anawajibu wa kununua taa za nishati ya jua zinazouzwa na kampuni hiyo ambayo ina mawakala mjini na vijijini kwani lengo lao ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma Salama bila kupata madhara ya kuunguliwa nyumba zao.
0 Comments