Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo ametoa wiki moja kwa mgodi wa Barick North Mara kuwasilisha nyaraka za mkataba wa ujenzi wa bwawa jipya la kuhifadhia maji yenye sumu yanayotokana na uchakataji wa dhahabu baada yamaagizo ya serikali.
“Katika ujenzi wa bwawa jipya kuna mambo yamekuwa hayatekelezwi, zimekuja kamati nyingi katika eneo hili nakutoa maelekezo lakini hayatekelezwi niwambie mimi si Waziri mnayemfikiria sitaki uzembe katika maagizo yangu," amesema Jafo.
0 Comments