KATIBU MKUU AHITIMISHA ZIARA JIMBO LA MUHAMBWE.
Tarehe 19/4/2021, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu @adoshaibuado alihitimisha ziara yake kwenye Jimbo la Muhambwe kwa kutembelea Kata za Busagara, Nyaruyoba na Busunzu.
Kwenye ziara hiyo Katibu Mkuu amekutana na Viongozi wa Matawi na Wanachama kwenye vijiji mbalimbali.
Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kujibu maswali, kutoa ufafanuzi na kusikiliza maoni ya wanachama kwenye ngazi ya matawi kuhusu ujenzi wa Chama.
Katibu Mkuu amewapongeza Wanachama kwenye matawi kwa moyo wao wa kujitolea kujenga Chama. Katibu Mkuu amewakumbusha wanachama hao kuwa nguzo muhimu ya ACT Wazalendo iliyokiwezesha Chama kustawi ni moyo wa kujitolea pamoja na viongozi na wanachama kuishi kindugu.
Kwenye ziara yake ya siku tatu, Katibu Mkuu ametembelea Kata 14 za Jimbo la Muhambwe.

0 Comments