Wanacheza kibingwa
✍🏼Simba walionesha sura mbili katika aina yao ya uchezaji , kwa dakika 45 zote mbili . Kipindi cha kwanza waliweza kuwafungua Kagera kupitia katikati kwa pasi fupifupi , kubadilishana nafasi uwanjani ( rotation ) na kukabia juu haraka mpira wakipoteza ( Counter Pressing ) . Viungo watatu washambuliaji wa Simba nyuma ya Mugalu ndio ilikuwa shida kwa “ BACK FIVE “ ya Kagera . Kipindi cha pili walilazimishwa kuzuia na walizuia vizuri kwa kipindi kirefu
✍🏼Chama Jr aliamua kucheza kwa mwendo wake , akiamua kuongeza kasi kwa kushambulia alifanya akiamua kupoozesha anafanya , ubongo wake unafanya kazi haraka sana . Goli la kwanza aliamua kuwafanya wachezaji wa Kagera kama “ Koni “ za mazoezini kabla ya Miquissone kufunga .
✍🏼Nilipenda pia goli la pili . PASS and MOVE . Mzamiru anapiga pasi ya mbele , Dilunga one touch kwa Miquissone , kondeboy anaachia tena na Dilunga anaweka njiani ...Mugalu kambani . Combination ya wachezaji wanne tu dhidi ya 7 goli linafungwa
✍🏼Pongezi kwa Kocha Baraza , alibadilisha mfumo kutoka “ BACK 3 “ kwenda “ BACK 4 “ ili kuongeza kiungo mshambuliaji mmoja nyuma ya straika , walifanikiwa kumiliki mpira kutokana na idadi nzuri ya wachezaji hasa wakivuka mstari wa katikati na kufanya Lwanga na Bwalya kuzuia eneo kubwa la uwanja .
✍🏼Tangu mwishoni mwa msimu uliopita na msimu huu pia mambo mawili tu Abdul Kassim akiboresha atakuwa kiungo mzuri zaidi ya sasa : MOJA : Kupiga zaidi pasi za mbele kwa haraka bila kuzunguka sana ( Quick vertical passes ) MBILI : Kunusa hatari haraka na kuhakikisha position yake mara nyingi ni mbele ya mabeki wawili wa kati .
NOTE :
1: Wawa + Onyango + Manula jinsi wanavyoongea kwa kuelekezana nyuma ndio msingi mkubwa wa Simba SC .
0 Comments