"Na ninaposema kuilea ATCL kimkakati ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kutoa unafuu wa madeni na baadhi ya kodi na tozo kama inavyofanyika kwenye nchi nyingine ili liweze kukua na kuweka mahesabu yake sawa, kwa sasa halina thamani lakini ni kwa sababu ya kurithi madeni makubwa ya nyuma"
"Kama serikali tunakwenda kulitua mzigo mkubwa
ATCL ili liweze kukua, tutajitahidi kuepuka mambo
yote yasiyo na tija kwa shirika letu, hatutakubali
kuona shirika linaendelea kupata hasara baada ya
uwekezaji mkubwa tuliofanya" - Rais
@samia_suluhu_hassan
"Kwa upande wa usafiri wa anga tutaendelea kujengaviwanja vya ndege ikiwemo cha Kimataifa cha Msalato hapa Dodoma na tutaendelea kulilea shirika letu la ndege ATCL kimkakati ili liweze kujiendesha.
kwa ufanisi" - Rais @samia_suluhu_hassan
"Kwa miaka hii mitano, tutaendeleza yaliyoandikwa kwenye llani ya Uchaguzi ya CCM, tutakamilisha ujenzi wa bandari, madaraja makubwa kama ya Kigongo Busisi na Tanzanite, tutaendelea na ujenzi wa reli pamoja na barabara mbalimbali" - Rais @samia_suluhu_hassan
0 Comments