Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS SAMIA: ASILIMIA 65 YA WATANZANIA NI WAKULIMA LAKINI KILIMO KINACHANGIA ASILIMIA 27 PEKEE

"Asilimia 65 ya Watanzania ni wakulima lakini kilimo kinachangia asilimia 27 pekee, na hii inaonesha kwamba tija katika sekta ya kilimo ni ndogo sana" 

Tutafanya maboresho ya sheria, sera zinazoleta vikwazo katika uwekezaji nchini, tutachukua hatua madhubutu kuboresha mazingira ya biashara, kutoa vivutio kwa wawekazaji wa kimkatiki ili uwekezaji ufanyike kwa haraka 

“Tutarudisha imani ya Wawekezaji na kutoa vivutio kwa Wawekezaji, tunalalamikiwa sana, kumekuwa na mchakato mrefu Watu wanapotaka kuwekeza Tanzania, Serikali ya Awamu ya Sita tunakwenda kukomesha hili na Uwekezaji utakwenda kwa haraka”———Rais Samia

"Tumedhamiria kufanyia mapitio ya jumla katika mashirika ya umma, ili kuwezesha mashirika hayo yanajiendesha, kwani mashirika mengi yanasuasua na pale inapofika kipindi cha kutoa gawio serikalini Bodi huzunguka huku na huko kwa kuhofia nafasi zao pale wasipotoa" 

''Watanzania wachache ndio wanaolipa kodi, hivyo kuna haja ya kutanua wigo wa walipa kodi, ningependa kuona wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wanalipa kodi bila shuruti na bila matumizi ya nguvu wakitambua kwamba kodi ni maendeleo yao'' 

"Tunakusudia kuelekeza nguvu kubwa katika ukuzaji wa Uchumi, Taifa letu limepata mafanikio makubwa kiuchumi hususan miaka 5 iliyopita. Takwimu zinaonyesha kwa Tanzania Uchumi wetu tumeusimamia kwa wastani wa 6.9% na kudhibiti Mfumuko wa Bei kwa 4.4%," -Rais Samia

“Tutafanya mabadiliko pale itakapobidi kwa lengo la kukuza ufanisi na dira, mpango wa tatu wa maendeleo, ajenda ya dunia ya malengo endelevu ya mwaka 2020. Katika hilo mtakumbuka akizindua Bunge hili Hayati Magufuli yapo mambo aliyoyasema narudia tena tulikuwa kitu kimoja.

Post a Comment

0 Comments