Advertisement

Responsive Advertisement

RAIS SAMIA: ILI KUINUA SEKTA YA KILIMO HATUNA BUDI KUIFUNGAMANISHA NA SEKTA YA VIWANDA, KWA MAANA KWAMBA MALIGHAFI NYINGI HUTOKANA NA KILIMO

"Ili kuinua sekta ya kilimo hatuna budi kuifungamanisha na sekta ya viwanda, kwa maana kwamba malighafi nyingi hutokana na kilimo" Rais Samia

“Tunalenga kuachana na uchungaji wa kuhama hama kwani hauna tija, katika miaka hii mitano tutawekeza katika kutoa elimu ya ufugaji wa kisasa na kuongeza uzalishaji wa vyaula vya mifugo viwandani,” – Rais Samia Suluhu 
 
''Sekta ya kilimo kwa sasa inachangia asilimia 100 ya chakula kinacholiwa nchini, asilimia 60 ya malighafi za wiwandani, asilimia 27 ya pato la taifa na asimilia 25 ya fedha za kigeni, hata hivyo bado sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi'' - Rais Samia

  Takwimu zinaonesha Chumi nyingi duniani zimeathiriwa na Corona, Tanzania nayo imeathirika kwa kushuka kwa Uchumi kutoka wastani wa 6.9% hadi 4.7%

 Wataalamu wa Uchumi wanatuambia Uchumi wetu unatakiwa kukua angalau kwa wastani wa asilimia 8 kwa mwaka

 Kununua meli nane za uvuvi ili kushiriki uvuvi wa bahari kuu, ambapo meli nne zitafanya kazi Zanzibar na nne upande wa Tanzania bara- Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan 

''Katika miaka mitano tunayokwenda nayo tutaendelea kuongeza nguvu kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, ikiwemo kuwa na mbegu bora, kuboresha afya ya udongo, pamoja na kuziwezesha taasisi za kilimo kwa kuzipa fedha ili ziweze kuzalisha kwa tija'' -Rais Samia

Post a Comment

0 Comments