Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania imekuwa ikilalamikiwa kwa kukosa mazingira mazuri ya uwekezeji ikiwemo sera zisizotabirika na urasimu. Serikali ya awamu ya sita inakusudia kumaliza hilo ili kurejesha imani kwa wawekezaji.
"Nchi yetu imekuwa ikilalamikiwa huko nje katika suala la uwekezaji, huku changamoto mbalimbali zikitajwa ikiwemo Sera zisizotabirika, urasimu, utaratibu wa kawaida usio wa kawaida wa kikodi. Serikali ya Awamu ya Sita inakwenda kuboresha hayo yote" Rais @SamiaSuluhu
"Ndani ya nchi yetu kumekuwa na mzunguko mrefu pale watu wanapokuja kuwekeza, serikali ya awamu ya sita inakwenda kulimaliza hilo" Rais Samia
Hatutakuwa tayari kuvumilia uvivu, uzembe na ubadhirifu wa mali au fedha za umma na kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuvutia zaidi wawekezaji- Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
"Mwaka jana mwezi Julai Taifa letu liliingia katika kundi la nchi za uchumi wa kati kwa kuwa na pato la wastani wa pato la dola za kimarekani 1080 kwa mtu mmoja zaidi ya kigezo cha kuingia katika kundi la nchi hizo cha wastani wa pato la dola za kimarekani 1036"Rais Samia
“Takwimu zinaonyesha uchumi dunia umeshuka kwa kiwango kikubwa kutokana na janga la corona, kwa Tanzania uchumi wetu umeshuka kutoka wastani wa asilimia 6.9 hadi 4.7,” – Rais Samia Suluhu
" jambo la kwanza katika uongozi wake ni kuendelea kudumisha tunu za taifa la Tanzania, yaani amani na utulivu na kudumisha muungano wa taifa hilo"
0 Comments