Advertisement

Responsive Advertisement

KIMBUGA JOBO: UMMA, WAVUVI WATAHADHARISHWA ZANZIBAR


Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Visiwani Zanzibar imetoa tahadhari kwa Umma na Wavuvi juu ya kuwepo kwa kimbunga Jobo.

Taarifa iliyotolewa na Kamisheni hiyo leo Alhamisi Aprili 22, imesema kuwa:

"Kufuatia taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) juu ya kujitokeza kwa mgandamizo mdogo wa hewa ambao umefikia kiwango cha kimbunga hafifu kinachojulikana kwa jina "Jobo" maeneo ya Kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar kilichopo katika bahari ya Hindi.

"Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kimbunga hicho kipo umbali wa Kilomita 930 na kilomita 1,030 kutoka pwani ya Mkoa wa Lindi na Mtwara ambacho pia kinaweza kusababisha ongezeko la upepo mkali na mawimbi ya bahari katika maeneo hayo.

"Hivyo, Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa inawataka wanandhi wakiwemo wavuvi na wamiliki wa vyombo vya usafiri baharini kuchukua tahadhari juu ya muelekeo wa Kimbunga hich," imeeleza taarifa hiyo ya Kamisheni na kuongezea kuwa:

"Aidha, Kamisheni kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kanda ya Zanzibar itaendelea kuwataarifu wananchi juu ya muelekeo wa kimbunga hicho kadri ya hali itakavyokuwa inaendelea.

"Kwa vile Zanzibar ni visiwa vilivyomo ndani ya bahari ya Hindi, kimbunga hiki kinawezekana kupita katika maeneo hayo," imeeleza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments