Advertisement

Responsive Advertisement

TANZANIA KUACHANA NA UFUGAJI WA KUHAMAHAMA


"Kuhusu ufugaji, kama nilivyowahi kusema, tunalenga kuachana na uchungaji wa kuhamahama.

"Katika kutimiza azma hii, tutaelekeza nguvu kubwa katika kuhamasisha ufugaji wa kisasa.

"Tutajielekeza kwenye uzalishaji kwa njia ya uhamilishaji kwa lengo la kubadili kosaafu (breed) ya mifugo yetu, ili kuwawezesha wafugaji kuwa na mifugo michache yenye sifa za uzalishaji mkubwa uwe wa Nyama au Maziwa na kuongeza tija.

"Tutaongeza vituo vya kuzalisha mbegu bora na pia kuongeza uzalishaji wa chakula cha mifugo viwandani kutoka tani 900,000 hadi tani milioni 8, kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani yetu ya Uchaguzi.

"Vilevile, tunakusudia kuongeza maeneo ya ufugajikutoka hekta 2,788,901 za sasa hadi hekta 6,000,000. Lengo ni kupunguza tabia ya sasa ya wafugaji kuhamahama, ambayo inasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira pamoja na
kuzusha migogoro kati yao na wakulima," Rais Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments