ANAANDIKA SHAFFIH DAUDA ✍

Kwa haraka unaweza kudhani ni mafundi gereji wametoka zao kupiga spana pale Tabata Dampo, huenda walikuwa wanashusha Injini ya Trekta unaweza ukahisi, ila sio kweli na achana na hisia hizo

Kwa haraka unaweza kudhani ni Wakulima wametoka zao kulima ngapa pale Mavimba mkoani Morogoro na sasa wanaenda kunywa togwa ila so kweli achana na hisia hizo kabisa

Pengine labda ni watoto wa shule ya Msingi Rubwe pale Kiwira Mkoani Mbeya? Hapana sio kweli kwa maana Mbeya haina Kidogo kichanga, hawawezi kuchafuka hivyo, sio kweli achana kabisa na hisia hizo

Pengine labda utasema ni Wakulima wa ndizi wametoka zao shambani huko Biharamulo mkoani Kagera, ila sio kweli hata Wahaya wenyewe hawatokubali, watasema migomba yao inapaliliwa na trekta kutoka Cologne Ujerumani, sahau hisia hizo

Atapita Mtu mmoja mjuvi kweli wa soka na atasema, hao ni wafanyakazi wa Jiji la Dodoma! Tutashtuka na kuuliza kivipi? Lakini swali letu Halina maana, kwani hatufahamu kuhusu kasi ya serikali? Basi hata hawa Watumishi wanapaswa kupambana

Mpita njia na mjuvi wa soka atasema hao ni Wanandinga wa Dodoma Jiji tena ilikuwa siku moja kwenye Derby ya Dodoma, hapo wanafanyia kazi mshahara unaotokana na Mama zetu pale Chinangali wapika wali, kodi za Bodaboda wa Majengo, sio rahisi bwana

Nimeipenda sana picha hii nami nikirudi nyumbani Bukoba nitabeba picha hii, nitaijengea frame na kusubiri Wajukuu zangu na kuwaambia kuwa "Wanaume wameumbiwa mateso na mateso ni kama haya mfano wake" mfanowe ndio huu

Lakini Wajukuu usikute kuna Mmoja kati yao alipotoka kwenye mechi akakutana na text ya Mkewe inasema "Endelea na Umalaya wako", mwingine atakuta "Ukimalizana nao niambie" na wa mwisho atakuta "Tuma na ya kutolea"

Asante sana FOOTBALL, asante sana MPIGA PICHA, Asanteni Dodoma JIJI @dodomajijifootballclub

FOOTBALL BLOODY HELL✊ Massive Respect to The beautiful GAME

No comments