MJADALA▪️Ukiitazama Orodha ya wafungaji bora kwenye VPL mpaka sasa, majina matatu utakayokutana pale juu ni
1: Meddie Kagere (Mabao 11)
2: Prince Dube (Mabao 11)
3: John Bocco (Mabao 10)
Kitu cha kufurahisha hapa.. Kagere ameyafunga mabao hayo katika dakika 954 tu (Wastani wa mechi 10)
Prince Dube amecheza dakika 1612 (Wastani wa mechi 17)
John Bocco amecheza DAKIKA 602 TU. Dakika chache zaidi. Wastani wa mechi 6 tu.
Mpaka sasa Ligi inaingia mzunguko wa 28. Kwa raundi 27 kuna timu zimeshacheza dakika 2430.
Nipe MAONI yako, kitendo cha kuwa na wafungaji bora WATATU waliocheza Dakika chache, kinatoa taswira gani kwa Ligi yetu na Wachezaji wetu?
0 Comments