KESHA LA ASUBUHI
JUMAMOSI, APRILI, 24, 2021
SOMO: KANUNI YA ASILI NA UZIMA
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
3 Yohana 1:2
Maelfu, naam mamilioni wanaotembea duniani wanataabika kutokana na mienendo yao mibovu. Je! wale ambao Kristo alitoa maisha yake kwa ajili yao wasingeithamini furaha yao, amani na afya yao kwa kutii sheria za asili? Sisi tu mali ya Bwana kwa uumbaji na kwa ukombozi na anahitaji tujifunze namna ya kuijali miili yetu, kwa kutii sheria ya uzima, afya na usafi.
Ni jukumu letu kutunza na kuheshimu miili yetu, ili kwamba tusiifanye kuwa ya uovu, uchafu na ya kuchukiza mbele za Mungu kwa kutokujali, anasa, tamaa na uchu tukafa wakati maisha yakiendelea.
Ni kwa uimara na uangavu kiasi gani rehema na huruma za Mungu zinang’aa katika kushughulika na warithi Wake... Mbingu yote ina shauku ya kina juu ya hali yetu njema ili kwamba Shetani asitutawale na kutufanya tukubaliane na tabia yake. “kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. 2 Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia lenye kuponya katika mbawa zake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama wa mazizini.” (Malaki 4:1, 2) ...
Kwa kudharau kanuni ya asili, wanaume na wanawake wanaweka misingi ya taabu na mateso. Kupitia udhaifu wao wa utashi wanakuwa watumwa kabisa wa uchu. Baadhi wanajichimbia kaburi kwa meno yao wenyewe; wengine wananajisi roho na mwili na kudhoofisha uwezo wa ubongo kwa kujisalimisha katika tabia mbaya ya uchafu wa maadili.
Kwa kufanya hivi wanajifungia milango ya jiji la mbinguni kwani adhabu ya kanuni zilizovunjwa ni lazima itambulike. Hukumu lazima ije... Kuna masomo ya kujifunza katika hili, kama yatatiiwa yataleta afya ya mwili na akili. Kama tabia ya ulaji na unywaji zitatawaliwa kwa hekima ya uwakala wa kibinadamu, na kula na kunywa kwa utukufu wa Mungu, maisha yake yatarefushwa. Kula uishi, usiishi ili kula.
Manuscript 53, April 24, 1896,, “A Knowledge of Physiology Necessary in Education.”
0 Comments