WIZARA YA ELIMU IMEWATAKA CHUO KIKUU CHA HURUIA KUENDELEA NA MASOMO

SERIKALI YAJIBU WARAKA HUU WA CHUO KIKUU HURUIA KUHUSU COVID-19,WANAFUNZI WA CHUO KIKUU HURIA WATAKIWA KUENDELEA NA MASOMO

Wizara ya Elimu imewataka Wanafunzi na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria kuendelea na masomo na kazi kama kawaida ikisema Waraka wa tahadhari ya COVID19 uliotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho ni batili.

Imeelezwa, Waraka wa Prof. Elifas Tozo Bisanda ni mawazo yake binafsi na hayakuzingatia Mwongozo wa Wizara ya Elimu wa Mei 27, 2020 kuhusu Udhibiti wa Maambukizi ya Ugonjwa wa Corona katika Shule, Vyuo na Taasisi za Elimu.

Aidha, Wizara hiyo pia imetoa rai kwa Taasisi za Elimu kuzingatia maelekezo ya Serikali kuhusu udhibiti wa maambukizi ya Ugonjwa huo.

Kwenye Waraka wa Prof. Bisanda, Wanafunzi wanaoingia katika Chuo hicho walisisitizwa kukaa nyumbani na kusoma kwa mtandao. Pia, tahadhari ilitolewa kwa wanaokusudia kusafiri nchi za nje ikielezwa siyo salama sana.
#BinagoUPDATES

No comments