MECHI ZOTE MBILI ZA NAMUNGO FC KUPIGWA TANZANIA, CAF WAAMUA ... ✍

CAF WAAMUA MECHI ZOTE ZICHEZWE TANZANIA BAADA YA SEKESEKE LA NAMUNGO FC

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika @caf_online limeamua mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na @namungofc ya Tanzania zichezwe nchini Tanzania.

Uamuzi huo umefanywa baada ya Kamati ya CAF ya Mashindano hayo kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyokuwa ichezwe Februari 14 nchini Angola.

Mechi zote mbili zinatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.
#BinagoUPDATES

No comments