MBUNGE WA MUHAMBWE ATASHASTA NDITIYE AFARIKI DUNIA MAPEMA ASUBUHI HII

#TANZIA

Mbunge wa Muhambwe (KIGOMA), Mhandisi Atashasta Nditiye ambaye amewahi kuhudumu kama Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi akishughulikia Mawasiliano amefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa bungeni na Spika wa Bunge, Job Ndugai imethibitisha. 

Spika Ndugai ameeleza kuwa Nditiye alipata ajali siku ya Jumatano tarehe  10 Februari na alipatiwa matibabu katika hospitali ya General Dodoma kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa ambako alifariki Dunia leo saa 4 asubuhi. 

#pole kwa Familia, Bunge na wote walioguswa na msiba huu

#KutokaBungeni
#HABARI #BinagoUPDATES

No comments