LESONI, FEBRUARI 15
SOMO: UWEPO, NENO, NA KAZI YA KUTENGENEZA BARABARA. (ISA. 40:3—8)
Ni kwa namna gani watu wa Mungu wanapokea faraja? (Isa. 40:3—8)
Mjumbe asiyetajwa jina anatangaza kwamba Mungu anakuja kuudhihirisha utukufu wake (Isa. 40:3—5). Sauti nyingine inatangaza kwamba ijapokuwa wanadamu ni wa kitambo tu kama majani, “neno la Mungu wetu litasimama milele” (Isa. 40:8).
Baada ya uhamisho, watu wa Mungu walijipatia tena kile walichokipokea katika Mlima Sinai na kukikataa kutokana na uasi wao, uliosababisha wao kuadhibiwa: uwepo wa Mungu na Neno Lake. Hivi ni sehemu za msingi za agano la Mungu na Israeli, vilivyohifadhiwa katika hekalu lake katikati yao (Kutoka 25:8, 16). Kwa kuwa walilihalifu neno lake, Mungu aliliacha hekalu lake (Ezekieli 9—11), lakini anarudi. Uwepo wake na Neno lake la kutegemewa milele huleta faraja, ukombozi, na tumaini.
Maandalizi gani ni ya muhimu kwa ajili ya ujio wa Bwana? Isa. 40:3—5.
Haifai kwa mfalme kutikiswa na barabara mbovu. Kwa hiyo ujio wake unatanguliwa na matengenezo ya barabara. Zaidi sana kwa Mfalme wa wafalme! Ujio Wake, unavyoonekana toka mashariki, ambako amekuwa uhamishoni na watu Wake kama hekalu kwao (Eze. 11:16), ungehitaji upangwaji upya wa mandhari. Ujenzi halisi, barabara kuu yenye ulinganifu kupitia katika vilima vya mawemawe mashariki mwa Yerusalemu vingekatisha tamaa, hata kwa baruti na buldoza. Ni Mungu pekee ndiye awezaye kuifanya kazi; ni Yeye ageuzaye “mahali palipopotoka kuwa panyofu” (Isa. 42:16). Lakini hahitaji barabara halisi kwa ajili ya usafiri kwa sababu ana gari linalopaa angani la makerubi (Ezekieli 1, 9—11).
Agano Jipya kwa wazi hutumia unabii wa Isaya kwa utengenezaji wa njia ya kiroho uliokamilishwa kupitia kwa mahubiri ya Yohana Mbatizaji (Mt. 3:3). Ujumbe wake ulikuwa: “ ‘Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia’ ” (Mt. 3:2) na ubatizo alioufanya ulikuwa “wa toba iletayo ondoleo la dhambi” (Marko 1:4). Hivyo, matengenezo ya barabara yalikuwa ni toba, utayari wa kugeuka kutoka dhambini, ili kupokea faraja ya msamaha na uwepo wa Mungu.
Yeremia 31:31—34 ilitangaza ujumbe ule ule wa kiroho mara nyingi kwa mateka wa Yuda kuelewa asili ya kiroho ya matengenezo ya barabara kwa ajili ya Mungu. Katika kifungu hiki, Bwana anawaahidi mwanzo mpya wale wanaohiari: “agano jipya” ambapo anaweka sheria yake mioyoni mwao na kuahidi kuwa Mungu wao. Wanamjua na tabia yake, kwa sababu amewasamehe.
Soma kwa umakini Isaya 40:6—8. Ni tumaini gani, wewe unayetoweka kama vile majani, unaweza kujipatia kutokana na kile ambacho haya mafungu yanasema? Yanapaswa kutuonya dhidi ya kuweka tumaini letu katika nini?
0 Comments