KESHA LA ASUBUHI
JUMATATU, FEBRUARI, 15, 2021
SOMO: IBADA YENYE MAANA
Maana hapo palipo na wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Yakobo 3:16, 17.
Kuna kitu kimoja ambacho nimekifanyia maamuzi. Si wajibu wa watoto wa Mungu kubakia katika sehemu ya hali ya hewa yenye kuchukiza, na kufeli katika afya mara zote. Wengi wa ndugu zetu wamefanya hili na wamepoteza maisha yao. Unapokuwa katika eneo ambalo angahewa imejaa msuguano, wakati kazi ya mtendakazi inafanywa kuwa ngumu sana na wale ambao mara zote wanatenda kazi kinyume na jitihada zake na kutenda kwa hila ili kunufaika, hebu mtenda kazi na aende eneo lingine ambalo mazingira yanafaa zaidi kiroho, na anapoweza kuwa na matumaini zaidi ya mafanikio....
Tunapaswa kukumbuka kuwa katika kila eneo tunalofanya kazi kwa upande wa Bwana, tunafanya kazi kinyume na jitihada za mawakala wa kishetani. Umepitia katika majaribu; na utakuwa na majaribu utakayokutana nayo kwa kiwango kikubwa au kidogo, popote utakapokuwa, Shetani atatazama kila sehemu yenye udhaifu katika tabia yako, naye atapambana ili kutawala; bali hatuwezi kuthubutu kupoteza nafasi yetu ya kupata ushindi kwa upande wa Bwana. Daima tunakutana na adui, na tusipokuwa macho, tutapoteza fursa za thamani za kupata ushindi....
Taabu za wakati huu wa sasa ni za tofauti katika mtindo, lakini Kristo aliyapitia hayo, na hatupaswi kuwa katika kutokuwa na hakika. Ametualika, “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:28—30). Ahadi ni, “Nitakuwa pamoja naye taabuni” (Zaburi 91:15).
Oh! Yeye ni ngome na mnara wa ulinzi mrefu ulioje kwetu! Nimekuwa nikipitia huzuni nyingi kwa sababu wengine miongoni mwa wale ambao ... wana ushahidi kwamba Bwana ametumia wakala dhaifu kuelezea kweli kuu na za milele, wanageuka kutoka katika chemchemi zilizo hai na kwenda kwenye visima vilivyochongwa na kunywa katika chemchemi zilizovunjika. Moyo wangu una maumivu makubwa usiku baada ya usiku. Naweza kulala lakini kwa saa chache; kwa kuwa tafakari ya wale walio katika njia zisizo za kweli yanautesa moyo
0 Comments