amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Jumanne 02/02/2021
*NAMNA YA KULETA MATOKEO*
*Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa,wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.* Matendo ya Mitume 4:13
☄️ Wakati Kristo alipokuwa hapa duniani, hakuwaelekeza wavuvi kuacha nyavu na boti zao, na kwenda kwa walimu wa Kiyahudi ili kupata maandalizi kwa ajili ya huduma ya Injili. Akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliwaona “ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata. Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwa chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata." Mathayo 4:18—22
☄️ Huu utii wa mara moja, usio na swali lolote, bila ahadi hata moja ya ujira, hauna kifani. Lakini maneno ya Kristo yalikuwa mwaliko ambao ulidokeza yote aliomaanisha.Kulikuwa na mvuto wenye msisitizo katika maneno yake. Hakukuwa na maelezo marefu, bali kile alichosema kilikuwa na nguvu inayovuta...
☄️ Yesu angeweza kuwafanya hawa wavuvi wasio na hadhi, kwa muunganiko naye, kuwa njia ya kuwatoa wanadamu katika kumtumikia shetani, na kuwafanya waumini katika Kristo, wakiwafundisha kuhusu ufalme wa Mungu. Katika kazi hii wangekuwa wahudumu wake, wavuvi wa watu...
☄️ Kristo alichagua mambo ya kipumbavu ya dunia hii —wale ambao dunia iliwatangaza kama wasiosoma na wasio na utambuzi —ili awaaibishe wenye hekima wa dunia. Wanafunzi wa Yesu hawakuwa wasomi wa mapokeo ya walimu wa Kiyahudi, bali pamoja na Yesu kama mfano wao na mwalimu, walikuwa wanapata elimu ya kiwango cha juu; kwa kuwa walikuwa na Kielelezo cha kiungu mbele yao. Kristo alikuwa anawasilisha kwao kweli za tabia za juu sana.
🔘 *Wale ambao Mungu anawatumia kufanya kazi kwa ajili yake, anawafanya wastahili kwa namna yake kwa ajili ya kazi hiyo. Wale wanaomhubiri Kristo sharti wajifunze kwa Kristo kila siku, ili kuelewa siri ya kuokoa na kuhudumia roho ambazo alikufa kwa ajili yake... Ni sharti wafuate kielelezo chake katika mambo yote, wakishiriki na wengine huruma yake na ukali wake dhidi ya matendo yote maovu.*
*🚨UMEJIFUNZA NINI?🚨*
Post a Comment