UTATA KIFO CHA MUUZA CHIPS

MAMBOSASA -TUNACHUNGUZA BADO KIFO CHA MUUZA CHIPSI, Wakati mwili wa Yusuf Deus (26) ukitarajiwa kusafirishwa leo kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili ya maziko, Jeshi la Polisi limesema bado linaendelea na uchunguzi wa kifo hicho"

Kauli hiyo ya polisi imekuja ikiwa tayari familia na Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama, Eliona Kimaro wakielezea sintofahamu ya tukio hilo"

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kujua tukio hilo huku akibainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea"

Tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili na pindi utakapokamilika tutakuwa na la kusema kwa vyombo vya habari,” alisema Mambosasa."
#BinagoUPDATES

No comments