CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI MPYA

Christiano Ronaldo  aweka rekodi mpya!

Mchezaji kandanda wa  Ureno na klabu ya soka ya Juventas Christiano Ronaldo  anazidi kuandikisha historia  na kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mtu  wa  kwanza duniani kufikisha wafuasi milioni miambili na hamsini katika mtandao wa  instagram. Christiano  ambaye hivi majuzi alijinyakulia ubingwa wa  kuwa mchezaji bora wa  karne hii, anazidi kujizolea umaarufu kila kona ulimwenguni"

Ronaldo alishawahi kuichezea timu  ya Manchester united ya Uingereza, Real Madrid ya Uhispania na sasa yupo nchini Italia akichapa kabumbu ya kulipwa kupitia klabu yake  ya Juventus ambayo inafanya vizuri sana na imekua ikitegemea sana huduma za nyota huyu wa  kutoka nchini Ureno. Mara nyingi Ronaldo amekua akishindanishwa na mchezaji wa  Argentina  na klabu ya Barcelona- Lioness Mess ambae pia anang'ara sana haswa kwenye ulingo huu wa  mchezo wa  kabumbu."
#BinagoUPDATES

No comments