unabii sehemu ya 2

UNABII:Sehemu ya pili.

MNYAMA DUBU
...........................
Danieli 7:5
Natazama mnyama mwingine wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwemo kinywani mwake katika meno yake, wakamwambia mnyama huyo hivi, inuka ule nyama tele.

                          DUBU
                ..............................
Dubu anawakilisha ufalme wa wamedi na waajemi. Esta 1:1-3

Umedi na waajemi ndio ufalme uliofuata baada ya kuanguka kwa babeli. Danieli 5:30-31.

Umedi na Uajemi ni sawa na kifua na mikono ya sanamu aliyoota nebukadreza. Danieli 2:39.

Mbavu 3 midomoni mwa mnyama dubu huwakilisha majimbo matatu ambayo utawala wa wamedi na waajemi uliyateka kwa ukatili, yani Babeli, Lidya, na Misri.

Dubu huyo ameinuliwa upande mmoja ikiwa na maana kwamba Uajemi ilikuwa na nguvu zaidi kuliko wamedi.

Wamedi na waajemi walitawala dunia kuanzia mwaka 539bc hadi 331bc..

No comments