JPM; HATUTARAJII KUJIFUNGIA NDANI KISA CORONA TUOMBE MUNGU ANATUONA, TANZANIA HAKUNA CORONA
"Kuna magonjwa yanajitokeza tokeza kama Corona, sisi Watanzania hatujajifungia ndani na hatutegemei kujifungia ndani na wala sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yupo hai na ataendelea kutulinda Watanzania,"
“Mtatishwa sana Ndugu zangu Watanzania, simameni imara, najua wapo baadhi ya Watanzania hata wameondoka Nchini na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa, na walikochanjwa huko wamekuja huku wametuletea Corona ambayo ni ya ajabuajabu, Simameni imara Chanjo hazifai,”
"Tutafanyiwa majaribio ya ajabu ambayo yataleta madhara makubwa, tuendelee kuchukua tahadhari za kiafya lakini tujihadhari sana tumeweza kukaa zaidi ya mwaka hatuna Corona na hata hapa hakuna aliyevaa barakoa, Mungu wetu yupo mbele ya shetani,"
"Niiombe Wizara ya Afya isiwe inakimbilia mambo ya machanjo chanjo bila yenyewe kujiridhisha. Ipo nchi fulani walichanjwa watoto wake wa kike, wanaambiwa ni kwa ajili ya kuzuia cancer ya kizazi, imekuja kugundulika ile chanjo ilikuwa ni ya kuwazuia wasizae" - Rais Magufuli akizungumza katika uzinduzi wa Shamba la miti Silayo Mkoani Geita Januari 27, 2021
JPM.
#BinagoUPDATES
Post a Comment