ROSE MUHANDO AFUNGUKA MAZITO
ROSE MUHANDO AFUNGUKA MAZITO;"
NILIKUWA NAITWA SHADYA KABLA YA KUITWA ROSE MUHANDO- malkiarosemuhando
Kabla ya kuitwa Rose Muhando nilikuwa naitwa Shadya kutoka Kilosa, kwetu mimi ni mtoto wa mwisho, toka nilivyozaliwa ilikuwa kila mwenzi naongezewa damu na hali iliyopelekea kuwa dhaifu sana na nilipofika miaka 9 hali ilikuwa mbaya na nilizunguka kote kwa waganga na sikupona ila tulikuwa na jirani yetu alikuwa ni mtu ambaye ameokoka na akawa ananiomba na napata nafauu"
Kuna siku niliwaambia wazazi wangu waniache nife na nikataka kulala chumba cha peke yangu na saa tisa usiku niliona mwanga ambao ulikuwa na rangi saba na niliona mkono mweupe umenigusa na ukasema"
Mimi ni Yesu nimekuponya na amka ukanitumikie' na nilipona saa hiyo hiyo na nikarudi shule na ile sauti ikawa inanirudia mara kwa mara, hivyo ilibidi nibadili dini na nikaokoka japo familia yangu haikutaka sababu nimetoka kwenye familia ya kiislam na Baba yangu alikuwa shekhe Mkuu Kilosa hivyo haikuwa rahisi"
MANENO YA ROSE MUHANDO AKIHOJI.
Post a Comment