MKUU WA WILAYA IRAMBA MHE. EMMANUEL LUHAHULA AMEWATAKA WANAFUNZI WOTE KULIPOTI SHULENI MAPEMA

Mkuu wa wilaya ya Iramba mhe Emmanuel Luhahula amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato Cha kwanza kuripoti shuleni Mara shule zitakapofunguliwa  na kuwataka wazazi/walezi kuhakikisha wanawapa mahitaji yote muhimu kwa ajili ya shule.
Mkuu wa wilaya ya Iramba ameyasema hayo wakati akitoa salamu za  sikukuu ya krismas na Mwaka mpya.Katika salamu hizo amewataka viongozi wote wa serikali za vijiji na kata kuhakikisha wanalisimamia suala hili kwa umakini na uadilifu na endapo watashindwa kusimamia hili ifikapo tarehe 16.2.2021 atachukua hatua Kali kwa viongozi hao,Pia amezitaka shule kulima mazao angalau hekari moja ya mahindi au mtama  pamoja na viazi lishe kwa ajili ya chakula Cha mchana kwa wanafunzi.

Amewakumbusha maafisa elimu kata,walimu wakuu na wakuu wa shule kuhakikisha wanasimamia majukumu yao na kuwashirikisha wananchi kushiriki katika  kuleta maendeleo ngazi ya shule na kutoa ushirikiano kwa kuhakikisha suala la lishe shuleni linafanikiwa kwa ushiriki wao Kama wadau muhimu wa elimu.

#HABARI #BinagoUPDATES 

No comments