amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Jumanne 29/12/2020

*NITAKUTANA NA MALAIKA MWANGALIZI WANGU*

*Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.* Mathayo 18:10

📚 Mpaka pale majaliwa ya Mungu yatakapoonekana katika nuru ya milele ndipo tutakapoelewa tunavyomwia kwa ajili ya usalama wetu na uingiliaji kati wa malaika wake watakatifu.

📚 Viumbe wa kimbingu wamekuwa wakitenda kazi katika mambo ya wanadamu. Wamekuwa wakitokea katika mavazi yang'aayo kama radi; wakija kama wanadamu, katika namna ya watembea kwa miguu. Wamekuwa wakipokea ukarimu katika nyumba za wanadamu; wamekuwa wakiwaongoza wasafiri nyakati za usiku. Wameharibu kusudi la mharibifu, na kutupilia mbali pigo la mharibifu.

📚 Ingawa watawala wa dunia hii hawalifahamu hili, mara nyingi katika mabaraza yao malaika wamekuwa wazungumzaji. Macho ya kibinadamu yamewatazama. Masikio ya kibinadamu yamesikiliza miito yao. Katika kumbi za mabaraza na mahakama za haki wajumbe hawa wa kimbingu wamekuwa wakitetea haki za wanaoonewa na kunyanyaswa. Wamekwamisha mipango na kuzuia mabaya na mateso kwa watoto wa Mungu

📚 Kila aliyekombolewa ataelewa huduma ya malaika katika maisha yake mwenyewe. Malaika ambaye alikuwa kiongozi katika maisha yake ya mwanzo kabisa; malaika aliyetazama hatua zake, na kufunika kichwa chake katika siku ya hatari; malaika aliyekuwa naye katika bonde la uvuli wa mauti; aliyeweka alama ya mahali alipozikwa, ambaye alikuwa wa kwanza kumsalimu katika ile asubuhi ya ufufuo itakuwa ni furaha kiasi gani kufanya mazungumzo pamoja naye, na kujifunza historia ya uingiliaji kati wa Mungu katika maisha ya mtu, na ushirikiano wa kimbingu katika kila kazi ya kibinadamu!

🔘 *Mashaka yote ya uzoefu wa maisha yatafunuliwa. Mahali tulipoonekana kuwa na mashaka na kukata tamaa, makusudi yaliyovunjwa na mipango iliyoharibiwa, itaonekana kuwa mikubwa, na ikitawala, kusudi la ushindi, upatanifu wa kiungu.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments