MGOMBEA URAISI UGANDA ANYUNYUZIWA PILIPILI
Mgombea urais Uganda anyunyuziwa pilipili;"
Mgombea wa urais kupitia chama cha Forum for democratic change FDC, Patrick Amuriat, amenyunyuziwa pilipili machoni kiasi cha kulazwa hospitalini"
Msafara wa Amuriat ulizuiwa na polisi alipokuwa safarini kwenda katika mkutano wa kampeni wilyani Tororo"
Amuriat, alifungua dirisha la gari lake kuzungumza na polisi, kwenye barabara ya Bugiri kuelekea Tororo, na ndipo afisa wa polisi, Abraham Asiimwe alipochukua fursa hiyo kumnyunyuzia pilipili machoni"
Tume ya uchaguzi imepiga marufuku kampeni katika wilaya ya Tororo, ambayo wachambuzi wa siasa Uganda wanasema ni ngome ya mgombea huyo wa upinzani"
Tume hiyo inasema wilaya ya Tororo ina maambukizi mengi ya virusi vya Corona na kampeni haziweki kufanyika wilayani humo"
Nyumbani kwa Amuriat ni wilayani Tororo."
Post a Comment