CCM; TUNAMSUBIRI MEMBE AAMUE

CCM: TUNAMSUBIRI MEMBE AAMUE;"

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinasubiri uamuzi wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Bernard Membe, aliyesema Januari, mwakani atatangaza rasmi kujiondoa upinzani.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu Oktoba 28, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii zikimhusisha Membe kutangaza kujiondoa rasmi katika chama hicho, Januari mosi, 2021.

Membe alikuwa miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo ya urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu kupitia Chama cha ACT-Wazalendo na kushika nafasi ya tatu kwa kupata kura 81,129 sawa na asilimia 0.5.

Katikati ya kampeni za uchaguzi huo, uongozi wa juu wa Chama cha ACT-Wazalendo kilitangaza kumuunga mkono aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Tundu Lissu.

Kutokana na hatua hiyo, Membe aliibuka na kusema kwamba hakuwa anatambua uamuzi uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na kwamba yeye ndiye alikuwa mgombea halali wa nafasi hiyo kupitia ACT-Wazalendo.
#BreakingNews #BinagoUPDATES

No comments